Jumatano, Septemba 10, 2014

HABARI NA PICHA KUHUSU AJALI YA BASI LA SUPER FEO ILIYOUA NA KUJERUHI LEO

Mzimu wa ajali umezidi kula roho za watanzania na sasa watu 2 wameripotiwa kufa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa, baada ya basi la Kampuni ya Super Feo aina ya Rosa kupinduka katika eneo la Sanangula nje kidogo ya mji wa Songea likitokea mkoani Ruvuma kuja  mkoani Mbeya.  
Taarifa ambayo Fichuo imezipata zimethibitisha kuwa waliokutwa na mauti katika ajali hiyo ni watu wawili, mwanamume na mwanamke ambao mpaka sasa hatujawafahamu kwa majina.
 Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa bado hakijafahamika. 

0 comments:

Chapisha Maoni