Kigogo wa mchezo wa Tennis duniani Roger Federer amefanikiwa kutinga kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya US Open inayoendelea mjini New York nchini Marekani.
Federer, anaeshika nafasi ya tatu kwa ubora wa duniani upande wa wanaume, amekamilisha azma ya kusonga mbele, baada ya kumshinda kwa shughuli pevu mpinzani wake kutoka nchini Ufaransa, Gael Monfils seti tatu kwa mbili ambazo ni 4-6, 3-6, 6-4, 7-5 na 6-2.

Haikuwa rahisi kwa Federer kufikia azma hiyo kwani ilimlazimu kufanya kazi ya ziada ya kumshinda mpinzani wake anaeshika nafasi ya 20 kwa uboera duniani, kutokana na kutanguliwa kwa seti mbili kwa sifuri.
Ushindi huo unampa wasaa Federer ambaye ni raia kutoka Uswiz, kukutana na Marin Cilic kutoka nchini Croatia, katika mchezo wa hatua ya nusu fainali.
Cilic amefanikiwa kutinga kwenye hatua hiyo baada ya kumshinda mpinzani wake kutoka nchini Jamuhuri ya Czech Tomáš Berdych, kwa jumla ya seti tatu kwa sifuri ambazo ni 6–2, 6–4 pamoja na 7–6.
Michezo mingine ya hatua ya robo fainali upande wa washiriki wa kiume kwenye michuano ya US Open ilishuhudia mshiriki kutoka nchini Serbia Novak Djokovic akimshinda Andy Murray kutoka nchini England kwa jumla ya seti tatu kwa moja ambazo ni 7–6, 6–7, 6–2 na 6–4
Naye Kei Nishikori kutoka nchini Japan alifanikiwa kutinga kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kumshinda mpinzani wake kutoka nchini Uswiz Stan Wawrinka, seti tatu kwa mbili ambazo ni 3–6, 7–5, 7–6, 6–7 na 6–4.

0 comments:
Chapisha Maoni