Shirika la afya Ulimwenguni WHO limeandaa mkutano wa
siku mbili unaoanza leo Geneva Uswis ukilenga kujadili uwezekano wa
matibabu dhidi ya ugonjwa wa Ebola.
Dawa zote zenye uwezekano wa kutibu ugonjwa huo zitajadiliwa na kufanyiwa uchunguzi wa kina wa maoni ya kitaalam.
Hata hivyo shirika la misaada la dawa MSF
limeonya kuwa huenda mkutano huo ukashindwa kuwa na matokeo makubwa
katika mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi ambako watu 1900
wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Mkuu wa shirika hilo la MSF Brice de la Vigne
akikosoa kuhusiana na mkutano huo amesema kuwa kilichopaswa kutiliwa
mkazo kwa sasa na mashirika ya kimataifa ni kuongeza idadi ya hospitali
dharula katika maeneo ya milipuko ya Ebola.




0 comments:
Chapisha Maoni