Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji
bora wa Uefa, na kuwapiku kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer na Arjen
Robben.
Ronaldo, 29, kutoka Ureno alipachika mabao 17 na kuisaidia Real Madrid kunyakua Kombe la Klabu Bingwa Ulaya - Uefa Champions League- msimu uliopita.
Ronaldo, 29, kutoka Ureno alipachika mabao 17 na kuisaidia Real Madrid kunyakua Kombe la Klabu Bingwa Ulaya - Uefa Champions League- msimu uliopita.
Nimefurahi sana, kwa hiyo lazima niwashukuru wachezaji wenzangu kwa sababu bila timu, tuzo binafsi ni vigumu kuzipata.
Amesema Ronaldo.
Ronaldo aliwazidi Neuer na Robben katika kura zilizopigwa na jopo la waandishi wa habari 54.
Neuer, 28, aliisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Dunia, huku Robben, 30, akifunga magoli 21 ya Bayern na matatu kwa timu ya taifa ya Uholanzi iliyofika nusu fainali Brazil.
Ronaldo alifunga mabao matatu -
hat-trick - wakati Ureno ilipoichapa Sweden katika mchezo wa kufuzu
kucheza Kombe la Dunia, ingawa hakuweza kuwika Brazil, kwani Ureno
ilitolewa katika ngazi ya makundi.Ronaldo aliwazidi Neuer na Robben katika kura zilizopigwa na jopo la waandishi wa habari 54.
Neuer, 28, aliisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Dunia, huku Robben, 30, akifunga magoli 21 ya Bayern na matatu kwa timu ya taifa ya Uholanzi iliyofika nusu fainali Brazil.
Hata hivyo, kiwango chake katika ngazi ya klabu kiliweza kushawishi jopo lililopiga kura, ambalo lilitakiwa kuchagua mshindi kati ya watatu hao baada ya mchujo kutoka wachezaji 10.
0 comments:
Chapisha Maoni