Jumatano, Agosti 27, 2014

ACHARANGWA HADI KUFA MKOANI MBEYA


Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Ibungu aliyefahamika kwa jina la Daud Paston (22) aliuawa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na mtu/watu wasiofahamika na kisha mwili wake kutupwa katika mto Lumbe.
Mwili wa marehemu ulikutwa na kutolewa katika mto lumbe uliopo katika kijiji na kata ya Ikuti, tarafa ya Ukukwe, wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya mnamo tarehe 26.08.2014 na ulikutwa na majeraha sehemu mbalimbali ya kuchomwa/kukatwa na kitu chenye ncha kali.
Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika japo taarifa za awali zinadai kuwa marehemu alikuwa na tabia ya wizi na ubakaji. Hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo na jitihada za kuwatafuta waliohusika zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mtu/watu waliohusika katika tukio hili azitoe katika mamlaka husika ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

0 comments:

Chapisha Maoni