Baraza kuu la kanisa la Kianglikana Uingereza, The General Synod, limeidhinisha wanawake kuwa maaskofu.
Maafisa katika kanisa hilo wanaamini wana ufuasi mkubwa unaounga mkono hoja hiyo.
Sasa baada ya kupitishwa kwa kura hiyo, huenda askofu wa kwanza mwanamke akachaguliwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Makasisi wanawake walio thuluthi moja ya
viongozi wa kidini wa kanisa la kianglikana, wanasema haki sawa
itawapandisha hadhi katika makanisa.
Hatua hiyo inemaliza mvutano wa miaka mingi na
kuvunja utamaduni wa makarne katika kanisa hilo. Tofauti nyingi
zimeibuka kuhusu suala hilo na hata kusababisha migawanyiko katika
kanisa hilo ambapo baadhi ya ma dayosisi yameshawatawaza maaskofu
wanawake, na kukaidi amri la hapo awali la kanisa kuu.
Nchi zilizo na maaskofu wanawake:New Zealand,Australia,Marekani,Canada na Afrika Kusini
'Msimamo wa viongozi wa kanisa hilo Afrika'
Kasisi Moses Bushendich kutoka kanisa la Kianglikana Uganda ameambia
BBC kuwa misimamo imegawanyika juu ya maaskofu wanawake kutokana na
mafundisho ya Bibilia.
Kanisa la Afrika halina uamuzi wa pamoja juu ya suala hili. Kila tawi limechukua msimamo wake baadhi wanapinga na wengine wanaunga mkono
amesema kasisi Bushendich.
Baadhi ya itikadi ambazo zimekuwepo kwa miaka m
ingi katika makanisa kuu kama vile Katoliki na Anglikana ni wanawake
kuwa maaskofu wanawake, na kruhusu ndoa ya wapenzi wa Jinsia moja ambayo
tayari baadhi ya maumini na maaskofu wa kanisa hilo wamepigia debe
kuidhinishwa.
0 comments:
Chapisha Maoni