Serikali ya Tanzania imelaani mauaji yanayofanywa na utawala haramu wa
Kizayuni wa Israel dhidi ya wakazi wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza,
huko Palestina. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo,
Bernard Membe ambapo pamoja na mambo mengine ameitaka jamii ya Kimataifa
hususan Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka kuzuia jinai hizo za
Wazayuni katika eneo hilo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania amekosoa
pia kimya cha walimwengu mbele ya jinai hizo ambazo zinakinzana na
sheria zote za kimataifa. Hiyo ni kauli ya kwanza kutolewa na nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, tangu kulipoanza mashambulizi
ya utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza siku nane
zilizopita.
0 comments:
Chapisha Maoni