Jumatatu, Julai 21, 2014

WALIMU WENYE DEGREE KUFUNDISHA SHULE YA MSINGI

Rais Jakaya Kikwete amesema kwamba kuanzia mwaka ujao walimu wenye Shahada (digrii) wataanza kufundisha Shule za Msingi. Hii ni kwa sababu kuna ongezeko kubwa la walimu wenye shahada wanaohitimu huku wakikosa nafasi za kufundisha katika shule za Sekondari.
Sera ya Elimu inatamka kwamba walimu wenye Cheti ndio hufundisha shule ya msingi lakini Rais Kikwete ameamua kufanya mapinduzi haya ili kuboresha kiwango cha elimu kinachozidi kushuka kila kukicha. Rais alitolea mfano kwamba ktk nchi zilizoendelea kama Uingereza walimu wenye digrii hufundisha hata katika shule za chekechea.
Haikuweza kufahamika mara moja kama walimu wametosha katika shule za sekondari, hasa shule za kata, hadi wapangiwe kufundisha shule za msingi.

0 comments:

Chapisha Maoni