INAVUTIA, baada ya kuisoma makala hii, hautaiangalia ndizi katika mtazamo wa awali.
Ndizi mbivu zina aina tatu ya sukari ambazo ni sucrose, fructose na
glucose pamoja Fibre (nyuzilishe). Ndizi zinakupa nguvu za papo hapo.
Utafiti uliofanywa umebaini ndizi mbivu mbili zinatosha kukupa nguvu
ambayo utaitumia kwa mazoezi ya dakika 90, ndio maana ni tunda namba
moja linalopendwa na wanariadha duniani.
Msongo wa mawazo
Kulingana na tafiti zilizofanyika hivi karibuni umebaini kuwa watu
wengi wanaopata msongo wa mawazo hujisikia vizuri wanapokula ndizi
mbivu.
Hali hii inatokana na ndizi kuwa na virutubisho aina ya Tryptophan
ambayo ni aina ya protini ambayo mwili huigeuza na kuwa Serotonin ambayo
kazi yake ni kukufanya upate utulivu na kuondokana na msongo wa mawazo.
Pia ndizi ina Vitamini B6 ambayo inasimamia usambazaji wa glucose au sukari mwilini, hivyo kusaidia kutuliza msongo wa mawazo.
Upungufu wa damu (Anemia)
Ndizi zina madini ya chuma na zinasaidia uzalishaji wa haemoglobin
ambayo ni mzalishaji mkuu wa damu mwilini, hivyo inawasaidia wale wenye
matatizo ya upungufu wa damu mwilini.
Presha ya Damu
Ndizi mbivu zina madini ya Potasium na ina madini ya chumvi kwa
kiwango cha chini, jambo linalofanya tunda hili kuwa dawa ya kupambana
na maradhi ya presha. Mamlaka ya Chakula na Dawa Marekani imetambua
uwezo wa ndizi katika, hivyo kuagiza wazalishaji na viwanda vya ndizi
kufanya tunda hili kuwa rasmi katika mapambano ya kupunguza vifo
vitokanavyo na presha na kiharusi (stroke).
Nguvu ya Ubongo
Utafiti uliofanywa Twickenham (Middlesex), Uingereza, umebaini
wanafunzi 200 walifaulu mitihani yao kwa kula ndizi mbivu katika milo ya
asubuhi na mchana. Ndizi imebainika kuwa na uwezo wa kuusaidia ubongo
kuongeza nguvu.
Utafiti huo pia umebaini madini ya Potassium yanaweza kusaidia ubongo kuwa na kasi na uwezo zaidi ya hali ya kawaida.
Kufunga Choo
Fiber (Nyuzilishe) inayopatikana kwenye ndizi mbivu inaweza
kuurejesha utumbo uliosababisha kufunga choo, kufanya kazi kama kawaida.
Madhara ya kilevi (Hangover)
Moja ya njia za haraka za kurudi kwenye hali ya kawaida baada ya
kupata Hangover hasa asubuhi ni kutumia ndizi au bidhaa zitokanazo na
ndizi kama Banana Milkshake. Ndizi hutuliza tumbo na inajenga au
kurejesha kiwango cha kawaida cha sukari mwilini huku ikirutubisha mfumo
wa maji mwilini.
Kiungulia
Ndizi zina uwezo wa kupambano na kemikali au acid zinazosababisha kiungulia.
Kuumwa asubuhi
Matumizi ya ndizi yamebainika kusaidia kuepusha kuugua asubuhi. Hii
inatokana na uwezo wa ndizi kuhimili kiwango cha sukari mwilini.
Alama za kung’atwa na Mbu
Wanaotokwa na vipele vyekundu baada ya kung’twa na mbu, ukifuta eneo
lenye kipele kwa upande wa ndani ya ganda la ndiz husaidia hupunguza
uvimbe na muwasho.
Neva
Ndizi zinasaidia sana kutibu mfumo wa neva.
Pia wenye matatizo ya uzito uliotokana na ulaji ama wanaokula vyakula
vyenye mafuta mengi, ndizi inaweza kukusaidia kuondokana na tatizo
hilo.
Utafiti uliofanywa kwa watu 5000, ulibaini kuwa walipata nafuu ya matatizo yao kwa kutumia ndizi kila baada ya saa mbili.
Vidonda vya tumbo (Ulcers)
Watu wenye matatizo kwenye utumbo, ndizi zinaweza kuwasaidia kutokana
na ulaini wake na hupunguza acid ambayo inasababisha vidonda tumboni.
Pia hupunguza maumivu kwa kuziba baadhi ya vidonda.
Kupunguza hali ya joto mwilini
Ndizi inasaidia kupunguza joto. Nchini Thailand kinamama wajawazito
hula ndizi, ili kuhakikisha wanawazaa watoto katika hali ya joto
pungufu.
Kula ndizi mbivu mara kwa mara, ili uepukane na matatizo mbalimbali ya kiafya.
0 comments:
Chapisha Maoni