Kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, amewapa matumaini zaidi Manchester
United baada ya kukiri kuwa "angependa kuichezea moja ya klabu kubwa
duniani" ingawa amesema hatolazimisha uhamisho wake (Independent) United
pia wamepata matumaini baada ya winga wa Real Madrid, Angel Di Maria,
26, kukataa kwenda Paris St- Germain (Daily Mirror), beki wa Atlètico
Madrid, Filipe Luis, 28, anajiandaa kufanya vipimo vya afya kabla ya
kuhamia Chelsea kwa ada ya pauni milioni
20 (Daily Express), boss wa Sevilla Unai Emery amesema anajiandaa
kumpoteza beki wake wa kushoto Alberto Moreno, 22, ambaye anasakwa na
Liverpool (Talksport), mshambuliaji wa Paris St-Germain Edison Cavani,
27, amemtaka wakala wake kumtafutia timu katika Ligi Kuu ya England (Sky
Sports), Arsenal wapo tayari kuacha kumfuatilia kiungo wa Real Madrid
Sami Khedira, 27, kufuatia kudai mshahara mkubwa. Khedira anataka kuwa
mchezaji anayelipwa zaidi Emirates (Daily Mirror), Arsenal wanaongeza
ufuatiliaji wa beki wa kulia wa Southampton Calum Chambers, 19, licha ya
kuwa wanakaribia kumchukua Mathieu Bebuchy, 28, kutoka Newcastle (Daily
Mail), beki wa zamani wa Manchester. United Rio Ferdinand, 35, atasaini
kuichezea QPR siku ya Jumanne (Sky Sports), Liverpool huenda wakipanda
dau la pauni milioni 44 kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco
Reus, 25, (Daily Express), Dynamo Moscow wamekubaliana na Marseille
kumsajili Mathieu Valbuena, 29, kwa pauni milioni 5.5. Arsenal,
Tottenham na West Ham zilikuwa zikimtaka pia (Talksport), Robin Van
Persie amepewa wiki tatu za kupumzika na Manchester United baada ya
Kombe la Dunia, huku Wayne Rooney wa Engalnd akitakiwa kuripoti kambini
mapema (Sun), kiungo wa Arsenal Jack Wilshire, 22, aliyeomba radhi mwezi
Oktoba kwa kuonekana akivuta sigara, ameonekana tena akifanya hivyo
mjini Las Vegas akiwa na Joe Hart (Daily Mail), Arsenal watataka Chris
Smalling kujumuishwa kwenye mkataba wowote iwapo Manchester United
watamchukua Thomas Vermaelen (Metro) Newcastle wamekamilisha usajili wa
Daryl Janmaat wa pauni milioni 5, kuziba nafasi ya Mathieu Debuchy
(Guardian).




0 comments:
Chapisha Maoni