Chelsea wako tayari kumuuza John Obi Mikel kwa pauni milioni 5 na klabu
kadhaa za Serie A za Italia zimeambiwa zinaweza kumchukua (Daily Mail),
meneja wa Manchester City, Manuel Pellegrini amekataa kuzungumza na
Chama cha Soka cha Brazil kuhusu kuchukua nafasi ya Luiz Filipe Scolari
kuifundisha timu ya taifa (El Mercurio), Real Madrid wamekubaliana na
James Rodriguez. Real Madrid wana subiri kukubaliana na Monaco wanaotaka
ada ya uhamisho kuwa euro milioni 80
(AS) West Ham watakamilisha usajili wa Enner Valencia siku ya Jumatano
kwa mkataba wa euro milioni 15 (Daily Mail), Swansea wamekataa pauni
milioni 8 zilizotolewa na Liverpool kumsajili Ben Davis (Daily
Telegraph), Manchester United, Chelsea na Arsenal watatakiwa kutoa zaidi
ya euro milioni 75 ili kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain,
Edison Cavani (talkSPORT), Everton wanakaribia kukamilisha usajili wa
kiungo wa Fevencvaros Muhamed Besic kwa pauni milioni 4 (Daily Mail),
Trabzonspor ya Uturuki wanamfuatilia beki wa Liverpool Kolo Toute (Daily
Mail), Newcastle wanakaribia kukamilisha usajili wa Emmanuel Rivière
kutoka Monaco (Daily Mail), hatua ya Manchester United kumtaka Arturo
Vidal kwa pauni milioni 35 kumesababisha boss wa Juventus kujiuzulu kwa
hasira (The Sun), Besitkas wanamtaka Demba Ba, 29, kwa mkopo huku
wakitaka kufanya uhamisho huo kuwa wa kudumu baada ya msimu (Daily
Mirror), AC Milan wanamtaka winga wa Manchester United Nani (Football
Italia), Manchester United wanawafuatilia kwa makini kuwapa majaribio
Joao Virginia, 15, aliyepewa jina la 'Cristiano Ronaldo mpya' na kipa
Joao Virginia, 15, kutoka Porto (Skysports)




0 comments:
Chapisha Maoni