Jumanne, Julai 08, 2014

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Miaka 58 iliyopita katika siku kama hii ya leo alifariki dunia mtaalamu, mwanafikra na mwandishi wa Kitaliano Giovanni Papini. Alizaliwa mwaka 1881 katika mji wa Florence nchini Italia. Giovanni alipitia kipindi kigumu cha utoto na ujana wake. Hata hivyo hamu kubwa ya masomo ilimpelekea kwenda katika maktaba za kijamii na kuzidisha elimu na taratibu alidhihirisha uwezo wake mkubwa katika taaluma ya fasihi. Msomi huyu ameandika vitabu vingi kama "A Man--Finished," "The Failure," na "Life of Christ,".
Siku kama ya leo miaka 20 iliyopita, alifariki dunia Kim Il-sung aliyekuwa Kiongozi na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomonisti wa Korea Kaskazini. Kim Il-sung alizaliwa mwaka 1912. Akiwa na cheo cha ukapteni jeshini alirejea kaskazini mwa nchi hiyo mwaka 1945 akiandamana na jeshi. Alipanda ngazi ya uongozi haraka na akachaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha wakomunisti wa nchi hiyo. Mwaka 1948 wakati nchi hiyo ilipoasisiwa na kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, Kim Il-sung alifikia cheo cha uwaziri mkuu. Katika vita vya Korea, Kim Il-sung aliteuliwa kuwa kamanda mkuu wa majeshi ya nchi hiyo na mwaka 1972 akawa rais wa taifa hilo.

0 comments:

Chapisha Maoni