Leo ni Jumanne tarehe 24 Ramadhani 1435 Hijria sawa na Julai 22, 2014.
Siku kama ya leo miaka 11 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 22 Julai 2003, waliuawa Uday na Qusay watoto wa Saddam Hussein dikteta wa zamani wa Iraq pambizoni mwa mji wa Mosul, kaskazini mwa Iraq. Uday na Qusay wakiwa wamefuatana na maafisa wa ngazi za juu wa Iraq walitoroka mjini Baghdad, baada ya majeshi ya Marekani na Uingereza kuishambulia nchi hiyo mwezi Aprili 2003. Majeshi ya Marekani yalishambulia nyumba walimokuwa wamejificha watoto hao wa Saddam Hussein na hatimaye kuwauwa pamoja na wasaidizi wao.
Tarehe 22 Julai 2002, ndege za kivita za utawala wa Israel zilishambulia eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina, na kuua watu 16 na wengine 150 kujeruhiwa. Shambulio hilo la kushtukiza lililofanyika usiku, lilisababisha liliua watoto 9 wasiokuwa na hatia yoyote. Hali kadhalika miongoni mwa waliouawa shahidi ni Sheikh Swalah Shahadah mmoja wa makamanda wa Brigedi ya Izzuddin Qassam akiwa pamoja na mke na binti yake.
Na siku kama ya leo miaka 53 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 22 Julai 1961, yalianza mapigano makali kati ya majeshi ya Ufaransa na Tunisia, baada ya vikosi vya Ufaransa kuishambulia bandari maarufu ya Bizerte iliyoko kaskazini mashariki mwa Tunisia. Mara baada ya Tunisia kujitawala kutoka kwa mkoloni Mfaransa mwaka 1956, mkoloni huyo aliendelea kuikalia kwa mabavu bandari ya Bizerte, na kuifanya kuwa kambi ya jeshi la anga la nchi hiyo. Hata hivy o majeshi ya Tunisia yalifanikiwa kuikomboa bandari hiyo kwenye mapigano hayo makali yaliyopelekea Watunisia 750 kuuawa.

0 comments:
Chapisha Maoni