Jumamosi, Julai 12, 2014

SUAREZ SASA MALI YA BARCELONA

Luis Suarez, amesaini mkataba wa miaka mitano na katalunya baada ya kukubaliana dili la Euro milioni 81 kutoka Liverpool. Pamoja na kuwa na kipengele cha Euro milioni 100 katika mkataba wake, Liverpool wamekubali kitita hicho pungufu ambapo Barca wametumia baadhi ya senti walizopata kutokana na mauzo ya Sanchez aliyetimkia Arsenal.
Suarez atasafiri kwenda Barcelona wiki ijayo kabla ya kutambulishwa rasmi siku ya jumatano, hata hivyo, kwa kuwa ana kifungo kutoka FIFA, hatapata utambulishi kama ule wa kawaida ndani ya Camp Nou. Hivyo basi, atatambulishwa kupitia shehemu maalum iitwayo Auditori 1899, ni mahali palipo karibu sana na uwanja huo wa Camp Nou.
Suárez atavaa uzi nambari tisa uloachwa na mchile Alexis Sanchez
Je, umeipenda biashara hii? Unadhani Barca watatisha zaidi? Au je? Huku Neymar, huku Messi, huku Suarez? Patamu si patamu hapo.

0 comments:

Chapisha Maoni