Bingwa mara tano wa kuogelea katika michuano ya Olimpiki duniani Ian
Thorpe amejitangaza hadharani kuwa ni shoga katika moja ya mahojiano
yake nchini Australia.
Awali Thorpe alikuwa akinakusha kuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kuandika maelezo yake mwaka 2012.
Muogeleaji huyo wa kutegemewa nchini Australia amekuwa akikabiliwa na msongo wa mawazo na kuwekwa Rehab mapema mwaka huu.
Katika moja ya mahojiano yake, Thorpe amesema kuwa hivi karibuni
amejisikia vizuri na kuona kawaida kuzungumza mbele ya marafiki zake
kuhusu jinsia yake.
0 comments:
Chapisha Maoni