Kampuni ya bidhaa za elektroniki ya, Samsung imesema
kuwa imepata ushahidi wa kuwatumikisha watoto kinyume na sheria katika
moja ya kiwanda cha kusambaza bidhaa zake nchini China cha Dongguan
Shinyang.
Samsung imesema kuwa iliichunguza kampuni hiyo
baada ya madai kutoka kwa shirika la kupambana dhidi ya utumkishaji wa
watoto ya Marekani 'China Labor Watch' kuituhumu kwa kuwatumikisha
watoto.
Awali
kampuni hiyo ya korea kusini ilikana kwamba baadhi ya kampuni
zinazosambaza bidhaa zake zinawaajiri wafanyakazi walio chini ya umri wa
miaka 16,lakini uchunguzi uliofanywa na shirika hilo umeilazimu kampuni
hiyo kukiri makosa yake.
Takriban watoto watano walio chini ya umri wa
miaka 16 walikuwa wakitengeneza baadhi ya sehemu za simu za samsung
,kulingana na uchunguzi wa siri wa shirika hilo la haki za
wafanyikazi,lililo na makao yake mjini New York.
Watoto hao ambao wamekuwa wakifanya kazi bila kandarasi wamekuwa wakilipwa thuluthi mbili za mshahara wa mtu mzima.
Wasambazaji wa bidhaa za Samsung wanashtumiwa
kwa kuvunja sheria za kazi za uchina kupitia kuwaruhusu watoto wadogo
kufanyakazi katika kemikali mbali na kupuuza sheria za uchina kuhusu
kazi za mda wa ziada ambapo hufanya kazi kwa masaa 11 katika zamu ya
masaa 10.
Hivi majuzi kampuni ya samsung ilitoa matokeo ya
ukaguzi wake kuhusu wasambazaji wa bidhaa zake nchini Uchina ambayo
hayakupata ushahidi wowote kuhusu ajira ya watoto.
kampuni hiyo imeahidi kukata uhusiano wake na kampuni za usambazaji wa bidhaa zake iwapo itathibitisha madai hayo mapya.
0 comments:
Chapisha Maoni