MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Winfrida Josephat
maarufu kama Rachel, amekanusha uvumi kuwa anatoka kimapenzi na mkongwe
wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’.Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT),
aliyetamba na kibao chake cha Kizunguzungu, alisema maneno hayo siyo
mageni kwake, lakini ukweli ni kwamba hawana uhusiano wa kimapenzi,
isipokuwa amemuweka katika mipango ya kuja kufanya kazi na mkali huyo wa
singo iliyotamba sana ya Zeze.
Aidha alisema katika maisha yake ya kila
siku, hategemei kuhongwa vitu au hela na wanaume, ila baada ya kupata
mafanikio kupitia sanaa, anaitumia kama mtaji wa kufanya shughuli
nyingine za kumuingizia kipato na hivyo kuwa na uwezo wa kukidhi
mahitaji yake.





0 comments:
Chapisha Maoni