Ndege ya Malaysia, Boeing 777 iliyokuwa inatoka Amsterdam
kwenda Kula Lumpur imeanguka Mashariki mwa Ukraine karibu kabisa na
mpaka wa Russia, leo, July 18.
Kwa mujibu wa CNN, waziri wa Malaysia anaehusika na mauala ya
Usafirishaji amesema kuwa abiria 280 na wafanyakazi 15 waliokuwa kwenye
ndege hiyo wamepoteza maisha.
Tweet ya Malaysia Airlines imeeleza kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano baada ya kutoka Amsterdam.
Kumekuwa na taarifa za awali kuwa ndege hiyo ilipigwa na na Ukraine, taarifa ambazo zimekanushwa na raisi wa Ukraine.
Rais wa Malaysia ameeleza kupitia twitter jinsi alivyosikitishwa na
tukio hilo na kudai kuwa wataanza uchunguzi wa tukio hilo haraka
iwezekanavyo kufahamu chanzo.
Tukio hili linatokea wakati ambapo bado ndege ya nchi hiyo, Flight 370 iliyopotea March 8 Mwaka huu bado haijapatikana.
0 comments:
Chapisha Maoni