RAIS Jakaya Kikwete ameagiza ifikapo Novemba mwaka huu, shule zote za
sekondari nchini, ziwe na maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi.
Ameagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanashirikiana na
wananchi ifikapo mwezi huo, kila shule ya sekondari katika maeneo yao,
inakuwa na maabara kwa ajili ya masomo ya Sayansi.
Alisema hayo katika nyakati tofauti akiwa wilayani Kilindi na Lushoto
kwenye ziara ya kikazi mkoani Tanga, iliyoanza Julai 8, mwaka huu
ikitarajiwa kuhitimishwa kesho.
Nataka ifikapo mwezi Novemba mwaka huu vyumba vya maabara viwe vimekamilika, tulipeana miaka miwili, imetimia
alisema.
Aliongeza,
lazima tusahihishe makosa tuliyofanya, ya kutojenga maabara wakati tunajenga shule za sekondari nchini kote.” Mwaka 2006 Serikali ilihamasisha ujenzi wa shule za sekondari nchini kote na mwitikio ni mzuri, lakini hakukuwa na uhamasishaji wa kujenga maabara.
Tumeamua kushughulikia suala la maabara ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa masomo ya sayansi kote nchini
alisisitiza.
Ubora wa elimu Rais alisema ameridhika na upanuzi wa elimu katika ngazi za Msingi na Sekondari kote nchini.
Alisema serikali inaendelea na hatua ya kutatua changamoto za ubora
wa elimu, kuongeza walimu, kuongeza vitabu, ujenzi wa maabara na nyumba
za walimu kote nchini.
Akihutubia mkutano wa hadhara wilayani Lushoto, Rais Kikwete aliahidi
kuboresha na kushughulikia ujenzi wa barabara ya kwenda Bumbuli na
kuhakikisha anaweka lami katika mji wa Lushoto na mji mdogo wa Bumbuli.
Rais anaendelea na ziara wilayani Lushoto na Mkinga, ambapo atazindua miradi na kukagua miradi ya maendeleo.




0 comments:
Chapisha Maoni