Takriban watu 18 wameripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea sokoni mjini Maiduguri Kaskazini mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC
kuwa gari lililokuwa limebeba mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa
liliwekwa ndani ya gari hilo.
Tukio hili linakuja huku ripoti ya hivi karibuni
ya jeshi la Nigeria ikisema kuwa limeshambulia moja ya ngome za kundi
la wapiganaji la Boko Haram.
Mwandishi wa BBC Habiba Adamu toka mji
mkuu wa Nigeria Abuja aliyetembeela eneo hilo anasema kuna utata wa
idadi ya waliouawa katika shambulio hilo kwani wakati wengine wakisema
waliouawa ni watano wengine wanasema huenda idadi ya waliouawa ikawa ni
zaidi ya hiyo iliyotolewa.
0 comments:
Chapisha Maoni