Watu sita wamefariki dunia na wengine wengi kuambukizwa ugonjwa
wa kipindupindu katika jimbo la Kano kaskazini mwa Nigeria. Abubakar
Labaran Yusuf Kamishna wa Afya wa Nigeria amesema kuwa watu sita
wamepoteza maisha kati ya jumla ya kesi 46 za maradhi ya kipindupindu
zilizosajiliwa hadi sasa. Kamishna wa Afya wa Nigeria amesema kuwa
sababu kuu inayosadikiwa kuwa chanzo cha maambukizo hayo ya kipindupindu
ni kuchafuka kwa maji.
Katika upande mwingine, taasisi moja ya kujitolea ya ISMA Medicare
Initiatives imedai kuwa watu waliokufa kutokana na maambukizo ya
kipindupindu ni kubwa zaidi ya hiyo iliyotajwa. Taasisi hiyo imesema
kuwa, watu 16 wamefariki dunia katika siku sita zilizopita. Surajo al
Kassim afisa wa taasisi hiyo ya ISMA Medicare Intitiatives amesema kuwa,
jumla ya watu 701 wameshambukizwa hadi sasa, huku wengine 20 wakiwa na
hali mbaya.
0 comments:
Chapisha Maoni