Jumatatu, Julai 21, 2014

KAMA NI WEWE UNGEFANYA NINI?

'Mimi nimeoa na katika ndoa yetu tuna mtoto mmoja wa kiume. Mwanzoni tuliishi vizuri sana na wife. Baada ya kazi kuharibika maisha yalibadilika sana na mambo yakawa magumu. Baadae mke aliongea na wazazi wake akampeleka mtoto kwao ili apate nafasi ya kujiendeleza kwa kozi fupi ya hotel management. Alivyomaliza akabahatika kupata kazi hotel moja hapa mjini. Mwanzoni alinidanganya kuwa ni meneja msaidizi lakni nilikuja kugundua sio kweli bali alikuwa upande wa bar counter.Nilianza kuona changes anaficha simu yake,dharau zikaanza nikajiuliza sana. Siku moja nilichukua simu yake usiku wa manane nikagundua ana mahusiano na watu wawili tofauti. Nilitulia kama wiki nzima nilipomhoji alikuja juu na hatimae ameondoka nyumbani, sasa ni miezi mitano. Ni mke wa ndoa tena ya kanisani, je nifanye nini?'

0 comments:

Chapisha Maoni