Rais Jakaya Kikwete ameagiza kukomeshwa biashara za magendo mipakani
na badala yake zifanyike biashara halali katika mipaka ya Tanzania na
nchi jirani ili kuwaondolea watu vishawishi vya kupita njia za panya za
kufanya biashara za magendo.
Rais Jakaya Kikwete ametoa agizo hilo baada ya kufungua soko la
kimataifa la Mkenda lililojengwa na mkandarasi mzalendo Bw. Charles
Mwansasu wa kampuni ya Nkemwa Tanzania Limited ya mkoani Ruvuma kwa
zaidi ya shilingi milioni 160 wakati akizungumza na wananchi wa mkenda
pamoja na wanamsumbiji waliokuja kumsikiliza wakitokea mji wa mpakani wa
Konglesi.
0 comments:
Chapisha Maoni