Jumanne, Julai 01, 2014

KESI YA DK. MAKOMGORO MAHANGA KIMEO!

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeifuta kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga dhidi ya mwanaharakati Kainerugaba Msemakweli kwamba ameghushi vyeti vya elimu.
Kesi hiyo ya madai namba 145/2009 ilifutwa baada ya Dk. Mahanga kushindwa kufika mahakamani mara zote ilipotajwa bila sababu.
Pamoja na Msemakweli, wadaiwa wengine ni mwandishi wa gazeti la Nipashe, Muhibu Saidi, Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo na Kampuni ya The Guardian Limited waliokuwa wakitetewa na wakili wa kujitegemea, Michael Ngaro.
Akitoa uamuzi huo, Jaji Salvatory Bongole, alisema sababu ni wakili wa mlalamikaji, Kennedy Fungamtama na Dk. Mahanga kutofika mahakamani huku kukiwa na ushahidi wa wao kuitwa mahakamani.
Kwa mujibu wa Jaji Bongole, ameifuta kesi hiyo chini ya amri ya tisa, kanuni ya nane ya sheria ya madai ya mwaka 2002.
Katika kesi hiyo, Dk. Mahanga aliomba wadaiwa wamlipe fidia ya sh bilioni tatu kutokana na athari za habari hiyo aliyodai kuwa ya uongo, ililenga kumshushia heshima yake hasa kwa kuwa ni kiongozi.
Habari hiyo iliyopewa kichwa kisemacho ‘Vyeti vya elimu: Mawaziri sita wanasa’ ilichapishwa kwenye gazeti la Nipashe la Oktoba 19 mwaka 2009.

0 comments:

Chapisha Maoni