Vikosi vya Israel vikisaidiwa na vifaru na ndege za kivita vimeingia
kwenye kingo za Ukanda wa Gaza katika operesheni kubwa ya kuangamiza
mahandaki ya Hamas ambayo kundi hilo limesema itashindwa.
Wakati mashambulizi hayo ya Israel kwa Gaza yakiingia siku yake ya 11
kwa jeshi la nchi hiyo kuushambulia ukanda huo wa mwambao kwa njia ya
anga na majini halikadhalika kwa kutumia vifaru viliyokusanywa mpakani,
idadi ya maafa ya Wapalestina imeongezeka na kupindukia 260.
Raia wamekuwa wakikimbia maeneo yenye kupakana na mpaka wa Israel ambapo
zaidi ya watu 30,000 wametafuta higadhi kwenye vituo vya Umoja wa
Mataifa. Miongoni mwa waliouwawa wakati wa mashambulizi hayo ya usiku ni
mwanajeshi mmoja wa Israel na mtoto mchanga wa miezi sita.
Taifa hilo la Kiyahudi limesema linaendelea na operesheni kuangamiza
mitandao ya mahandaki iliyojaa Gaza inayotumiwa na wanamgambo wa
Kipalestina kutengenezea maroketi na kuishambulia Israel. Katika hatua
isio ya kawaida Israel ilitangaza operesheni yake hiyo ya ardhini kabla
hata ya kuanza.
0 comments:
Chapisha Maoni