Jumanne, Julai 08, 2014

BOB JUNIOR AMBWAGA TENA MKE WAKE

Hit maker wa ngoma ya ‘Bashasha’ Raheem Rummy Nanji aka Bob Junior baada ya kurudiana na mkewe Halima Ally miezi kadhaa iliyopita kutokana na ndoa yao kuvunjika kwa sababu ya Bob Junior ku-cheat nje ndoa na kufumaniwa na vic***.
Kwa sasa mkali huyo ametoa tena talaka 3 kwa mkewe Halima kutokana na tetesi zilizopo chini ya carpet kuwa ndugu wa Bob Junior wanamuona Halima aka mama Rummy hana nyota angavu kwa mumewe kitu kinachosababisha Bob kufifia katika ramani ya kimuziki, Chanzo kikamvutia waya Bob Junior ili kuhakikisha ni kweli red card imetolewa tena?
CHANZO: Mambo vipi Bob Junior?
BOB JUNIOR: Poa niaje man.
CHANZO: Poa, nasikia umempiga chini mkeo?
BOB JUNIOR: Mimi nilikuambia sijawahi kurudiana naye tangu tulivyoachana mwanzo.
Ingawa wanamwagana ila wamebahatika kupata mtoto mmoja ‘Rummy’ mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kadhaa hadi sasa.

0 comments:

Chapisha Maoni