Jumanne, Julai 08, 2014

BAADA YA KIPIGO CHA 7-1, DAVID LUIS ANENA

Nahodha wa muda wa Brazil David Luiz amewataka mashabiki wa tim,u hiyo kote duniani kuwasamehe wachezaji waliokuwa uwanjani Selecao ilipoadhibiwa kichapo cha mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.

Amini Usiamini Ujerumani ilikuwa inaongoza mabao 5-0 kufikia dakika 29 ya kipindi cha kwanza .
Wajerumani walikuwa timu bora zaidi yetu
Luiz,ambaye alitajwa kama nahodha wa muda baada ya marufuku ya Nahodha Thiago Silva kumlazimu kutizama tu mechi hiyo alisema hawjui kilichotendeka lakini ni wakati wao kujifunza kutokana na aibu hiyo ya kusakamwa 7-1. "Ni siku ya majonzi tele kwa wabrazil''.

Mtuwieni radhi sijui tutafanya nini ilituwaone tena wabrazil wakitabasamu,?
Kilio kimezidi kote nchini humo haswa baada ya nyota wa Brazil Neymar kujeruhiwa uti wa mgongo Ijumaa iliyopita katika mechi ya kufuzu kwa nusu fainali dhidi ya Colombia.
Kwa Upande wake Kipa wa Brazil Julio Cesar alitaja dakika hizo kumi timu hiyo ilipofungwa mabao manne kuwa sawa na kuzimia.
''Sio jambo unaloweza kujieleza.

0 comments:

Chapisha Maoni