Watu wawili, baba na mwanawe, wamekufa baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Ikwiriri kuacha njia
na kugonga kingo ya Mto Kihoi na kupinduka.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei
alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 5:00 usiku, eneo la Kihoi Ikwiriri
na aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Ramadhani Nassoro
aliyekuwa dereva na mwanaye Abuu Ramadhani.
Matei alisema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka
kwa tairi. Alisema katika ajali hiyo, Samira Nassoro alivunjika mfupa wa
paja la kushoto na alipelekwa Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu
zaidi.
Kaimu mganga mkuu wa Kituo cha Afya cha Ikwiriri,
Edmund Masele alisema maiti zimekabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa
ajili ya maziko.
0 comments:
Chapisha Maoni