Jumatatu, Juni 30, 2014

UGIRIKI YAGOMA KUPOKEA POSHO

Huku timu za Afrika zikilazimika kusafirisha mamilioni ya dola za kimarekani hadi Brazil (Nigeria Cameroon) ilikuzima migomo kabla ya mechi muhimu timu ya Ugiriki ilifanya kinyume na hayo ilipokataa katakata kupokea malimbikizi ya marupurupu yao kutoka kwa serikali .
Timu hiyo iliyoondolewa na Costa Rica katika mkondo wa pili ilimwandikia waziri mkuu wa Ugiriki Antonis Samaras barua ikimtaka atumie fedha hizo kujenga uwanja mpya wa kandanda utakaotumika kutambua na kukuza vizazi vipya vya kandanda.
Ugiriki iliambulia kichapo cha mabao 5-3 kupitia mikwaju ya penalti mikononi mwa Costa Rica.
Bwana Samaras aliahidi kutekeleza ombi la wachezaji wake alipozungumza kwa njia ya simu na maafisa wa shirikisho la soka la Ugiriki.

0 comments:

Chapisha Maoni