Mwili wa marehemu Nasra ukiwa ndani ya jeneza ukiingizwa mochwari Morogoro |
MWILI wa mtoto Nasra Rashid (4) utaagwa katika
Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kuanzia saa 2 hadi saa 3 asubuhi leo.
Mwili huo baadaye utazikwa katika makaburi ya Kola, mkoani humo. Nasra
alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili Juni 1, mwaka huu akiwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akitibiwa baada ya kuugua
kutokana na kuishi kwenye boksi kwa muda wa miaka 4.
0 comments:
Chapisha Maoni