Jumatatu, Juni 02, 2014

BINDI ALIYEKUWA AISUBIRI KIFO HATIMAYE AMEFARIKI DUNIA

MIBURO Anne, msichana mwenye umri wa miaka 17 aliripotiwa katika gazeti moja la Udaku 27, mwaka huu likiwa na kichwa cha habari ‘NINASUBIRI  MUNGU AICHUKUE ROHO YANGU’, amefariki dunia wiki iliyopita akiwa njiani kurejea nyumbani kwao, nchini Burundi.Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akisumbuliwa na uvimbe mwilini, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako ugonjwa wake ulishindwa kutibika.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, mwanafunzi huyo alianza kuumwa tokea akiwa kidato cha pili, hali iliyomlazimu kuacha kwenda shule ili kufuatilia matibabu, ambayo yalimfikisha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kaka wa marehemu aliyetambuliwa kwa jina moja la Albert alisema mdogo wake alipoteza maisha wakiwa mpakani mwa nchi hizi mbili na kwamba alimhangaikia sana ili aweze kupona licha ya uwezo wake mdogo kifedha.

0 comments:

Chapisha Maoni