HUKU akiacha wake watatu, Yvonne-Sheryl Ngatikwa
‘Monalisa’, Beatrice na Lucy, msiba wa marehemu George Otieno ‘Tyson’
(41) umezua maajabu kwa kuwa na majeneza mawili.
Kwa mujibu wa chanzo, uwepo wa majeneza hayo ulitokana na kukosekana kwa
usimamizi imara kiasi cha kuyafanya yakosolewe kwa kukosa ubora
kulingana na hadhi ya marehemu na hivyo nusura linunuliwe la tatu.
JENEZA LA KWANZA
Jeneza la kwanza lilikuwa la
mbao bila ishara kwamba ni jeneza. Wengi waliliita sanduku kutokana na
muundo wake na lilifikishwa hospitali tayari kwa kuubeba mwili wa
marehemu.
JENEZA LA PILI
Msanii wa Bongo Fleva, Ambwene
Yesaya ‘AY’ alipofika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro alishtushwa
kuwepo kwa jeneza hilo hivyo alijitolea kwenda kununua jingine kwa
gharama ya shilingi 600,000.
Akizungumza Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
‘Taff’, Simon Mwakifwamba alikiri kuwepo kwa majeneza mawili lakini
akasema AY aliokoa jahazi kwa kununua la pili lenye ubora.
Hata hivyo, baada ya jeneza la pili kuufikisha mwili kwenye Hospitali
ya Kairuki jijini Dar, wasanii wa Bongo Movie walilipinga wakidai nalo
pia halikuwa na hadhi ya kubebea mwili wa Tyson hadi Kisumo, Kenya
ambako marehemu atazikwa.
Lile jeneza alilonunua AY nalo si bora sana ukilinganisha na majeneza ya marehemu Adam Kuambiana na Recho Haule. Tyson si mtu wa kumweka kwenye jeneza kama hili. Tutatafuta jingine lakini tutamwambia AY atusamehe
alisema Katibu wa Bongo Movie, William Mtitu.
Naye Mwakifwamba akizungumzia kuhusu kununua jeneza jingine na kuachana na lile lililosafirishia mwili kutoka Morogoro, alisema:
Kikao cha mwisho tumekubaliana kwamba, jeneza litumike lilelile la Morogoro ila lifanyiwe decoration (mapambo) ili liweze kuwa la kisasa zaidi.
MKUU WA WILAYA
Mwakifwamba alikwenda mbele zaidi kwa kusema, AY mbali na kununua jeneza lakini pia alinunua shati jipya la marehemu kufuatia T-shirt aliyoivaa siku ya ajali kujaa damu.
Mwakifwamba alikwenda mbele zaidi kwa kusema, AY mbali na kununua jeneza lakini pia alinunua shati jipya la marehemu kufuatia T-shirt aliyoivaa siku ya ajali kujaa damu.
Akaongeza:
Wa kuwashukuru ni wengi, mfano Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka yeye ndiye aliyetoa usafiri wa gari (Toyota Land Cruiser) kwa ajili ya kuleta mwili wa marehemu hapa Dar.
MWILI KUSAFIRISHWA KENYA
Naye ndugu wa marehemu Tyson, Felix Owino alipozungumza na Uwazi juzi alisema kikao cha familia kimeamua kuusafirisha mwili kwenda kuzikwa Kisumo, Kenya.
Naye ndugu wa marehemu Tyson, Felix Owino alipozungumza na Uwazi juzi alisema kikao cha familia kimeamua kuusafirisha mwili kwenda kuzikwa Kisumo, Kenya.
Alisema mwili utasafirishwa Jumanne (leo) au Jumatano kulingana na
kukamilika kwa bajeti ambayo ni shilingi milioni 19. Aliongeza kuwa,
mwili huo utaagwa kwenye Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam.
Marehemu Tyson alifariki dunia kwa ajali ya gari aina ya Toyota Noah,
Ijumaa iliyopita wakati yeye na wenzake wakitokea Dodoma kwenda Dar.
Wengine watatu walijeruhiwa na wanatibiwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili, akiwemo MC maarufu, Gladness Chiduo ‘Zipompa’.
Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Gairo kuelekea Morogoro. Marehemu ameacha watoto wawili.
Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Gairo kuelekea Morogoro. Marehemu ameacha watoto wawili.
0 comments:
Chapisha Maoni