Maelfu ya wenyeji wasio na makao mjini Sao Paolo
waliandamana nje ya uwanja utakaoandaa mechi ya kwanza ya kombe la dunia
alhamisi ijayo wakipinga gharama ya juu ya mashindano hayo.
Maandamano hayo yaliwadia siku moja tu baada ya
rais wa Brazil Dilma Rousseff kuwahakikishia wageni na mashabiki wa
kandanda kuwa kamwe hatoruhusu maandamano yatie doa kwenye kipute hicho
cha kombe la dunia.
Takriban waandamanaji 10,000 waliziba barabara
zote mjini Sao Paolo wakiishinikiza serikali ya bi Rousseff iwekeze
katika sekta ya afya elimu na ipunguze gharama ya juu ya usafiri wa
umma.
Zaidi ya watu milioni moja waliandamana katika
barabara za miji yote ya Brazil wakishinikiza serikali kupunguza
ubadhirifu wa fedha na kupunguza matumizi yake kwa maandalizi ya kombe
la dunia na yale ya Olimpiki yatakayofanyika mjini Rio mwaka wa 2016.
Licha
ya hakikisho la rais Rousseff wafanyikazi wa reli walitishia kuanza
mgomo upya huku polisi wa trafiki mjini Sao Paolo pia wakitishia kuanza
mgomo Alhamisi.
Mapema wiki hii serikali iliwaongezea polisi
wote mshahara ilikuzuia mgomo uliotishia kuporomosha hali ya utengamano
huku fainali ya kombe la dunia likinukia.
Serikali imeahidi kutumia polisi na hata jeshi la taifa kudumisha amani na utengamano wakati wa kombe la dunia.
0 comments:
Chapisha Maoni