Kwa
mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia, rangi itatumika na
waamuzi kuweka alama uwanjani wakati wa free kick. Rangi hiyo ambayo
hutengenzwa kwa kutumia zaidi maji, itatumika kuweka alama mahala hasa
kosa au 'foul' ilipotokea ili mpira uwekwe hapo bila kusogezwa. Pia
rangi hiyo itatumika kuchora mstari ambao timu inatakiwa
"kujenga ukuta". Hii itaepusha wachezaji kuusogelea mpira kabla free
kick haijapigwa. Rangi hiyo ni nyeupe na hufutika baada ya kama dakika
moja. FIFA iliidhinisha matumizi ya rangi hiyo katika Kombe la Dunia
2014, baada ya kutumiwa na kupata mafanikio katika Kombe la Dunia kwa
vijana chini ya miaka 20, mwaka 2013, Kombe la Dunia chini ya miaka 17,
mwaka 2013, na katika Kombe la Dunia la vilabu mwaka 2013.




0 comments:
Chapisha Maoni