Jumamosi, Juni 28, 2014

BAADA YA KUTIMULIWA MAN U SASA MOYES KUIFUNDISHA GALATASARAY

Aliyekuwa kocha wa Manchester United David Moyes ameahidiwa kitita cha pauni milioni £4 kwa mwaka ilikumrithi Roberto Mancini kama kocha wa Galatasaray ya Uturuki.
Iwapo mkataba huo utakubalika na ''The Chosen one '' huenda raia huyo wa Scotland akarejea katika safu ya ukufunzi miezi michache tangu atimuliwe huko Old Trafford kufuatia msururu wa matokeo duni.
Kibarua chake kiliota nyasi huko Old Trafford mwezi aprili Manchester ikiwa katika nafasi ya saba katika ligi ya Uingereza msimu mmoja tu tangu watwae ubingwa chini ya mkufunzi shupavu Sir alex fergusson.
Galatasaray imedhibitishia waandishi wa habari kuwa Moyes alizuru Istanbul ilikufanya mkutano na rais wa klabu hiyo Unal Aysal.

0 comments:

Chapisha Maoni