Juhudi za uokoji zinaendelea siku ya pili Kaskazini
mashariki mwa Afghanistan ambapo watu wapatao elfu mbili wanasadikiwa
kufa kutokana na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya vijiji kwenye mkoa
wa Badakhshan.
Vijiji hivyo vimefunikwa na udongo wenye ukubwa
wa karibu mita kumi kwenda juu baada ya sehem ya mlima mmoja kuporomoja
kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.
Udongo ulioporomoka na kufunika baadhi ya nyumba |
Baadhi ya watu wakiangalia kama wapo walio hai |
Miili ya watu wapata 350 imepatikana
hapo jana katika maporomoko ya ardhi kazkazini mashariki mwa taifa hilo
na hakuna mtu yoyote aliyepatikana akiwa hai.Umoja wa Mataifa unasema
karibu watu 4000 hawana makazi.
Mashirika ya misaada na uokoaji kwa sasa wameanza kuwapa mikate na
maji maelfu ya watu waliolala nje kwenye baridi kali wakiwa hawana
makazi.
Kuna taarifa nyingine zinazosema maelfu mengine
ya watu huenda wakawa wametoweka baada ya upande mmoja wa mlima
kuangukia kijiji k katika eneo la mashambani la mkoa wa Badakhshan
unaopakana na mataifa ya Tajikistan,Uchina na pakistan.
Waokoaji wamekuwa wakilalamika kuwa hawana vifaa vya kutosha kuwasaka manusura.
Mwandishi wa BBC mjini kabul anasema kuwa eneo
hilo ni miongoni mwa maeneo yenye umaskini mkubwa na katika taifa
maskini duniani na huenda ikachukua majuma kadhaa kabla ya serikali
kubaini ukubwa wa janga hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni