Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na silaha mbalimbali na nyama ya wanyamapori kinyume cha sheria.
Kamanda wa polisi mkoani Iringa Bw. Ramadhani Mungi amesema, Lusiano Ngweta miaka 35 na Abbas Williamu miaka 42 wamekamatwa na magobole mawili, vipande vya nondo 102, baruti gramu 20, fataki 12 na nyama ya digidigi kilo4.
Kamanda Mungi amesema, kwenye kijiji cha Ifeke, wilayani Kilolo mtu mmoja Ibrahim Chavalla miaka 70 ameuawa na watu wasiojulikana na kitu chenye ncha kali kwa tuhuma za imani za kishirikina.
Aidha, kwenye kijiji cha Ihomasa, wilayani Mufindi Amani Makoga miaka 25 amekamatwa na silaha aina ya Gobole bila kibali na askari wa hifadhi ya wanyamapori ya Ruaha.
Hata hivyo, kamanda Mungi amesema uchunguzi bado unaendelea ili watuhumiwa hao waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

0 comments:
Chapisha Maoni