Kitoto cha kike chenye umri wa saa 5 kimeopolewa kutoka shimo la choo na wasamaria wema katika mtaa wa Korongoni, Kata ya Holili jana jioni (Jumatatu Mei 5) na kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi wilaya ya Rombo kikiwa hai.
Shuhuda wa kwanza wa tukio hilo alisema wakati anapita akitokea katika mihangaiko ya kutafuta mkono uende kinywani alisikia sauti ya kichanga kikilia katika shimo lililofunikwa na miiba iliyokomaa.

Askari wa lituo cha polisi Holili akiwa na kichanga hicho baada ya kukifikisha hospitalini |
Shuhuda huyo ambaya hakutaka jina lake litajwe alisema ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada, na wasamaria wema walitokea kutoka nyumba za jirani ili kutoa msaada.
Balozi wa Mtaa wa Korongoni, Kata ya Maida-Holili, Barnabas Assenga maarufu kwa jina la Mzee Makeba alisema majirani walimfuata na alitoa ngazi kwa ajili ya watu kwenda kukiopoa kichanga hicho.
Mzee Makeba alisema baada ya kupewa taarifa hizo alitoa taarifa jeshi la polisi kwa msaada zaidi, na walifika kwa wakati kwa ajili ya kusimamia zoezi hilo.
Jeshi la Polisi lilipofika aliopolewa kichanga huyo na kuwahishwa katika Hospitali ya Huruma iliyopo wilayani Rombo kwa uangalizi.
Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Mama Hakini anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35-40 anatuhumiwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kwa kosa la kutaka kuua kwa makusudi.
Uchunguzi umebaini kuwa mume wa mwanamke huyo anafanya kazi Jijini Mwanza, na hajawaki kurudi Holili licha ya kuwa na mawasiliano mazuri na mkewe huyo.
Aidha chanzo kingine kilisema kuwa mumewe alikimbia kijiji hapo baada ya matatizo kumkuta katika kazi yake ya “ukuli”.
Hata hivyo kilibainisha kuwa mwanamume huyo alimtaka mama Hakini kuja na watoto mwanza ili waendelee na maisha yao lakini alikataa.
Pia uchunguzi huo umebaini kuwa mwanamke huyo amekuwa “kiruka njia” hivyo hata mimba aliyoipata ilitokana na tabia yake isiyoeleweka.
Mbali na hilo chanzo kingine kimejuza kuwa mwanamke huyo alishawahi kutoa mimba kadhaa hapo awali kwa ajili ya kutaka starehe za dunia hii.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wanawake wawe na huruma na watoto wao kwani ni kosa kisheria kutaka kuua, mwanamke huyo atapanda kortini kujibu mashtaka.

0 comments:
Chapisha Maoni