Mkataba wa usitishaji uhasama kati ya serikali ya
rais Salva kiir na waasi wanaoongozwa na Riek Machar nchini Sudan kusini
umeanza kutekelezwa mda mfupi uliopita .
![]() |
| Afisa wa umoja wa mataifa Navi Pillay akisalimiana na kiongozi wa waasi nchni Sudan Kusini Riek Machar. |
Msemaji wa rais Salva Kiir ameiambia BBC kwamba
vikosi vya serikali vina haki ya kulipiza kisasi iwapo waasi watakiuka
mkataba huo na basi kuvishambulia.
Hatahivyo msemaji huyo Ateny Wek Ateny amesema kuwa serikali ya Sudan Kusini haina mpango wa kuzua vita vyovyote.
Amekana kwamba vita hivyo vya miezi mitano vilibadilika na kuwa vya kikabila kati ya kabila la Dinka na Lile la Nuer.
Vita hivyo vimesababisha mauaji ya maelfu ya watu huku zaidi ya wengine millioni moja wakiwachwa bila makao.
Awali Umoja wa mataifa ulizitaka pande zote
mbili kusaidia katika kuhakikisha kuwa misaada ya dharura inawafikia
waathiriwa wa vita hivyo kufuatia kutiwa sahihi kwa makubaliano hayo.




0 comments:
Chapisha Maoni