Jumamosi, Mei 03, 2014

MAAJABU MENGINE, WAUMINI WALISHWA MAJANI KANISANI, WAPO WALIOPONA, WENGINE WAZIMIA

Ikiwa ni miezi miwili imepita tangu huduma ya Mtume Lesego Daniel wa nchini Afrika Kusini ya Rabboni Ministries Centre kuwa maarufu duniani baada ya waumini wake kula nyasi kama moja ya namna ambavyo roho mtakatifu alivyowaongoza, sasa waumini hao wamegeukia majani.
Imefahamika kuwa wamekuwa wakitumia njia hiyo kupata uponyaji licha ya watu wengi kupinga ufunuo wa namna hiyo.
Kupitia picha zilizotolewa na huduma hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook, zimeonesha waumini wakikimbilia matawi ya miti na kuanza kula majani yake, huku mmoja wao aliyefika kanisani hapo kwa mara ya kwawnza akidai kupona jino lililokuwa likimuuma.
Muumini huyo alisema kwamba alifika kanisani hapo kwa mara ya kwanza Ijumaa ya wiki iliyopita akiwa na dawa za kutuliza maumivu ambazo zilikuwa hazimsadii lakini alipokula tu majani yalimponya na kwamba akirudi nyumbani, mumewe (ambaye pia ni mtumishi) atafurahi sana kwa uponyaji huo.
Huduma hiyo imekuwa ikipingwa na watu wengi hasa baada ya tukio la waumini kula nyasi huku pia mtume huyo muda mwingine huwafanyia maombi waumini wake akiwa amewakanyaga migongoni.
Mtume Lesego Daniel
Licha ya kelele kutoka kwa viongozi wa dini na makanisa mbalimbali kuwakataza waumini wao na wakristo kuwa makini na huduma ya mtumishi huyo, ndiyo kama wamewaruhusu kwenda huko kwa kuwa inasemekana watu wamepagawa na baadhi yao huzimia wakati wa kupata maombi hayo katika huduma hiyo inayoendelea kujikusanyia waumini kila kukicha.
Huduma hiyo ilikuwa ikifanyika katika majengo ya Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Tshwane kwa sasa wamepata eneo lao ambalo wameliita shamba la Rabboni ambalo wanatarajia kuhamia huko kesho Jumapili.

0 comments:

Chapisha Maoni