Kampuni kubwa ya kutengeza magari nchini Marekani imeagiza magari milioni 1.4 yarejeshwe kutokana na hitilafu ya usukani.
Takriban magari milioni 1.1 yaliyoundwa kwa
mtindo wa kispoti yaliyokuwa yameuzwa Marekani Kaskazini yametakiwa
kurejeshwa kwani huenda yana hitilafu kwenye usukani.
Vilevile
magari mengine 200,000 yenye muundo wa Taurus yaliyoundwa kati ya mwaka
wa 2010 na 2014 huenda yakakumbwa na tatizo ya kushika kutu kwa haraka.
Matukio kama hayo yaliyofanyika majuzi huenda
yakaifanya kampuni hiyo kuvunja rekodi ya kutaka magari mengi zaidi
yarejeshwe katika kipindi cha mwaka mmoja.
Magari zaidi ya milioni moja yanahitilafu ya usukani
Urejesho huo umetokea wakati sakata ya usalama inawakumba wapinzani wakuu wa kampuni ya hiyo , General Motors (GM).
GM ililaumiwa kwa kutotoa ilani za kiusalama
kwamba baadhi ya magari yake hata baada ya kubaini kuwa magari hayo
yanazima ghafla.
Dosari hiyo imehusishwa na vifo 13, ingawa wasanifu wa Marekani wanaamini kuwa idadi hiyo itaongezeka.
Pindi tangazo hilo lilipofanywa, kampuni za
kutengeneza magari hayo pamoja na wasanifu wa Marekani wameongeza juhudi
za kurejesha magari ambayo yanapatikana kuwa na dosari.
0 comments:
Chapisha Maoni