Mwanamuziki Mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Diamond
Platinum ameahidi kuwatendea haki wakazi wa mikoa ya kusini kila mwaka
kwa kile anachodai mafanikio makubwa ya ndoto yake ya kuwa mwanamuzi
bora hapa nchini imeanzia mkoa wa Mtwara.
Mwanamuziki huyo aliambatana na kipenzi chake, Malkia wa Bongo
Movie nchini, Wema Sepetu – ‘Beautiful Onyinye’ au Madame kama mashabiki
wake walivyokuwa wakimuita amethibitisha kauli hiyo kwa mashabiki wake
waliofurika katika tamasha maalumu la Ties & Heels lililofanyika
katika ukumbi wa makonde beach Mkoani Mtwara na kudhaminiwa na kampuni
ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Amesema tangu kuanza kwake kujiingiza kuwa mwanamuzi wa muziki wa
kizazi kipya alianza kwa shoo yake mkoani mtwara ambapo ilionyesha
kuwakuna wapenzi wengi na aliendelea kujulikana maeneo mengi hapa nchini
kutokana na wapenzi walivyoanza kukumkubali, na ndipo aliwaahidi
wapenzi hao kuwa ataendelea kuwasili mkoani humo kila mwaka kwa kulipa
fadhila kwa mafanikio anayoyapata.
Akizungumzia juu ya shoo hiyo iliyokuwa ya kukata na shoka kwa wakazi
wa mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Kanda ya kusini wa Vodacom Tanzania, Henry
Tzamburakis amebainisha kuwa tukio hili limeandaliwa ikiwa ni sehemu ya
burudani kwa wateja wetu, kufurahi kwa pamoja na kuwashukuru wateja wetu
kwa kuendelea kutumia huduma zetu.
Hakuna kitu ambacho tunajali na kukithamini kama wateja wetu, haijalishi wawe kona gani ya Tanzania, walipo popote tutawafikia. Vodacom imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwa kipindi chote hicho watanzania wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya tuwe mtandao unaaongoza kwa mawasiliano nchini
Alisema Tzamburakis.
Kwa kuongezea Tzamburakis amewashukuru wakazi na mashabiki wote wa
Diamond na wapenzi wa muziki wa Bongo Flava kujitokeza kwa wingi kwani
mbali na burudani wamenufaika na baadhi ya huduma na bidhaa mbali mbali
za Vodacom.
Nae Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu alieambatana na mpenzi
wake alisema hakuona shida kumsindikiza asali wake wa moyo mtwara yote
haya kwaajili ya mashabiki wao. Kwa tafsiri nyingine mashabiki wa Mtwara
wanabahati kubwa ya kutembelewa nasi na tutadumisha utamaduni huu kila
mwaka.
0 comments:
Chapisha Maoni