Takriban watu 63 wamefariki baada ya treni iliyokuwa
imebeba abiria kupoteza mwelekeo Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo.
Msemaji wa serikali Lambert Mende alisema kuwa
polisi wanahofia kuwa idadi ya watu waliofariki huenda ikaongezeka. Pia
alisema kuwa polisi watafanya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali.
Treni hiyo ilikuwa imebeba idadi kubwa ya watu baadhi wakiwa wamekaa juu ya treni |
Treni hiyo ilikuwa imebeba idadi kubwa ya watu kupindukia wengine wakiwa wameketi juu ya treni yenyewe.
Waziri wa mambo ya ndani katika mkoa huo Jean
Marie Dikanga Kazadi, aliambia BBC kuwadereva wa treni hiyo alikuwa
anaiendesha kwa kasi .
Watu 80 walijeruhiwa vibaya huku wengine saba wakiwa bado wamekwama ndani ya treni vifusi.
Treni ilianguka Jumanne asubuhi lakini waokozi waliweza tu kuwasili nyakati za jioni.
Sehemu kubwa ya njia ya reli ya DRC, imesalia katika hali yake tangu enzi za ukoloni na ni nadra kufanyiwa ukarabati.
Treni hiyo ilianguka wakati dereva alipokuwa anajaribu kupunguza kasi.
0 comments:
Chapisha Maoni