Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
nchini Somalia, Nicholas Kay, ameshutumu mauaji ya washauri wawili wa
Umoja wa Mataifa ambao wamekuwa wakifanyakazi katika kitengo cha Ofisi
ya Umoja wa Mataifa kuhusu Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC).
Washauri hao wawili wa kimataifa walikuwa
Galkayo kusaidia jitihada za Ofisi ya UNODC katika eneo hilo wakati
walipouawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika uwanja wa
ndege wa Galkayo, Puntland, Somalia.
Umoja wa Mataifa umesema unawalaani wauaji hao.
"Wafanyakazi wenzetu wa Umoja wa Mataifa
walikuwa wakifanyakazi ya kuwasaidia wananchi wa Somalia kufikia ndoto
yao ya kuwa na taifa lenye amani na imara. Hakuna uhalali wowote wa
kufanyika shambulio hilo.
Natoa wito kwa serikali kufanya uchunguzi wa
kina ili kuwabaini wahalifu hao na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria
bila kuchelewa".Amesema Bwana Kay.
Nicholas Kay, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia.
"Natoa salamu zangu za pole kwa familia na marafiki wa watu hao waliouawa.
Umoja wa Mataifa umedhamiria kuendelea na msaada
wao wa dhati kwa wananchi wa Somalia ambao wanatoka katika mgogoro
uliodumu kwa miongo kadhaa," amesema Mwakilishi huyo Maalum wa Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Kay.
Habari kutoka Mohadishu, Somalia, zinasema
kikundi cha wapiganaji wa al-Shabab kimepongeza mauaji hayo na kudai
kufurahishwa na taarifa hizo za kuuawa kwa raia wa kigeni katika mji wa
Galkayo, katikati mwa Somalia Jumatatu.
"TUnapongeza na kufurahishwa na mauaji ya
maafisa wa Umoja wa Mataifa, leo. Mashirika ya Umoja wa Mataifa daima ni
maadui wa Waislam na Wasomali na vifo vyao vimelifurahisha kundi la
wapiganaji wa Mujahdeen" wamesema.
Walipoulizwa kama wanahusika na mauaji hayo, al-Shabab wamesema kwa sasa hawapingi wala kudai kuhusika na mauaji hayo”
0 comments:
Chapisha Maoni