Timu ya Taifa Ya Tanzania kwa Watoto wa Mitaani hatimaye Yanyakua
Kombe la Dunia Kwa Watoto wa Mitaani, (Street Child World Cup 2014) Rio
de Janeiro, Brazil
Ikitinga fainali za Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani kwa mara ya
pili mfululizo, hatimaye Tanzania imeweza kutwaa Kombe la Dunia kwa
Watoto wa Mitaani kama linavyojulikana Street Child World Cup hapa Rio
de Janeiro.
Tanzania leo imeweza kuchachanya Burundi iliyokuwa ikipewa nafasi
kubwa ya kulinyakua Kombe hili kwa Kuinyuka magoli 3 kwa moja huku
mchezaji kiungo mshambuliaji wa Tanzania Frank William akipiga magoli
matatu na kuwa nyota wa mchezo, Tanzania iliweza kufunga magoli mawili
kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuongeza goli latatu kipindi cha pili.
Burundi iliweza kufunga goli lake la pekee zikiwa zimebaki daika nne
mpira kuisha.
Tanzania imeweza kufika fainali baadaya kuonyesha kiwango cha juu
hata kuzishinda timu ngumu kama Burundi, Marekani, Indonesia, Nicarague,
Ufilipino na Argentina.
Golikipa wa Tanzania Emmanuel ameweza kuchaguliwa kuwa golikipa bowa
wa michuano hii ya kombe la dunia. Ikumbukwe kuwa fainali zilizopita za
michuano hii Kule Durban Afrika Kusini Tanzania ilifika fainali na
kufungwa na India.
Timu ya Tanzania itaondoka Brazil kesho Jioni ikipitia Dubai na
kuwasili Dar es salaam siku ya tarehe 10 kwa Shirika la Ndege la
Emirates.
0 comments:
Chapisha Maoni