Moto umeanza kuwaka kwa Halmashauri ya Mkoa wa Mbeya kwa kuwataka
watu kuacha tabia ya kufanya siasa kwa timu ya Mbeya City ili kuifanya
timu hiyo kuendelea kuwa na uhai.
Mbeya City imefanikiwa kumaliza Ligi ya Tanzania Bara huku ikishika
nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, huku Azam FC ikinyakua taji hilo
na Yanga SC kushika nafasi ya pili.
Kwa mujibu wa wadau wa soka mkoani Mbeya, watu wameanza kujipitisha
wakijinadi kuwa timu hiyo imefanikiwa kwa uwezo wao, wakati ni juhudi za
Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Katibu Tawala wa mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja, alizungumzia hilo
kwenye hafla ya kuwapongeza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa
timu ya Mbeya City.
Timu hiyo sasa imevunja kambi yao baada ya ligi kumalizika na kuiweka
timu katika mazingira mazuri ya kushiriki ligi ijayo kwa mafanikio.
Baadhi ya wanasiasa mkoani hapa wameanza kuyahusisha mafanikio ya timu hiyo na harakati zao za kisiasa za vyama vyao hali ambayo ni hatari kwa uhai wa Mbeya City katika ulimwengu wa soka nchini, maana huu sio mwendo mzuri.
Siasa wakati mwingine inaweza kuwagawa mashabiki wa timu hiyo kutokana na kwamba kila mmoja ana mapenzi na chama chake
alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mbeya City, Musa Mapunda, alisema
baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya tatu msimu huu, sasa wanaweka
mikakati ya kuhakikisha timu hiyo inachukua ubingwa wa ligi Kuu ya Soka
Tanzania bara msimu ujao.
Naye kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi, alisema vijana wake wamefanya kazi nzuri na watajiandaa vyema kwa ligi ijayo.
Mbeya City ilianzishwa Julai mwaka 2011 na huu ni msimu wake wa
kwanza kushiriki ligi hiyo na kupata mafanikio yak upigiwa mfano.
0 comments:
Chapisha Maoni