Jumatano, Aprili 09, 2014

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO MAREKANI KAMA RAIS BORA ZAIDI AFRIKA


RAIS Jakaya Kikwete ametunukiwa tuzo ijulikanayo kama Africa's Most Impactful Leader of the Year na taasisi moja ya Marekani yenye makao yake Washington D.C.
Taarifa ya serikali imesema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ndiye atapokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Kikwete.
Tayari Waziri Membe na ujumbe wame wamemwisha kuekea nchini Marekani ambako tuzo hiyo itatolewa Washington D.C, Aprili 9, 2014.
Taarifa iliyotolewa Jumanne Aprili 8, mwaka huu na Idara ya Mawasiliano ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imesema tuzo hiyo hutolewa kila mwaka na taasisi ya uchapishaji ya 'African Leadership Magazine' yenye makazi yake nchini Marekani kwa viongozi wa Afrika wanaofikia vigezo vilivyowekwa na taasisi hiyo.
Vigezo hivyo vimetajwa kuwa ni pamoja na kuzingatia utawala bora, demokrasia na kuheshimu haki za binadamu kwa mwaka 2013, ambapo kwa mwaka huu inatolewa kwa Rais Kikwete.
Kwa mujibu wa taasisi hiyo, tuzo hiyo inatolewa kwa Rais Kikwete kutokana na namna ya pekee ya uongozi wake wenye matokeo yanayopimika kiutawala bora, hususani kwa mwananchi wa kawaida wa Tanzania.
Aidha uongozi wake umeiletea Tanzania heshima kubwa kimataifa na kuiwekaTanzania kama chaguo muhimu kwa wawekezaji, kutokana na ukuaji uchumi na maboresho ya sera.
Tuzo hiyo imewahi kutolewa kwa Marais na viongozi wengine mbalimbali wa Afrika wakiwemo Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa Liberia, James Michel, Rais wa Shelisheli na Rais Mstaafu wa Ghana, John Koffor.
Ujumbe wa Membe utamhusisha Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Salvatory Rweymamu, waandishi wa habari na maafisa wa serikali, ambapo Waziri Membe atarejea nchini 11 Aprili, 2014.

0 comments:

Chapisha Maoni