Alianza kutangaza pale C2C kipindi cha ‘Radha Za Pwani’ na baadae kuhamia EA Radio na TV akitangaza kipindi cha ‘Tam Tam Za Pwani’,wakat huo huo alikuwa muimbaji wa taarab na alishapita katika vikundi vingi kama ‘Super Shine’, ‘Zanzibar One’, ‘Kasino’ na baadae alihamia ‘Jahazi Morden Taarab’.
Mwanne Othumani Kambi aka Mwa4 mtangazaji na muimbaji wa taarabu na miduara. |
Kwa sasa mwanadada huyo amekacha suala la uimbaji na kujikita zaidi katika utangazaji na uandaaji wa vipindi, akifunguka zaidi.
”Baada ya kupiga mzigo C2C kwa muda wa miaka miwili then nikahamia EATV na Radio, so kilichofanya niachane music wa taarab ni kukosa muda kutosha kabisa kutokana na majukumu kuwa mengi kazini so najikuta siwezi kuhudhuria mazoezi kabisa, mashabiki wangu wasijali kuimba kwenye miduara kama kawa so naomba wajue hivyo kwa sasa.”
Mwanne
0 comments:
Chapisha Maoni