ZIMEKATIKA wiki mbili tangu kuzikwa kwa mtoto Christian Alex (6)
aliyeuawa kwa kushambuliwa na mbwa watatu waliodaiwa ni wa Ubalozi wa
Qatar nchini, mbwa hao wamemkosakosa baba mtu.
Tukio la kuuawa kwa mtoto huyo lilijiri Kunduchi Jangwani Beach jijini Dar Machi 26, mwaka huu.
Tukio la kuuawa kwa mtoto huyo lilijiri Kunduchi Jangwani Beach jijini Dar Machi 26, mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo, mara baada ya kumaliza shughuli ya kumzika
marehemu katika Makaburi ya Mburahati jijini Dar, baba mzazi Alex
Augustino alikaa kikao na ndugu ili kuangalia uwezekano wa kufika kwenye
makazi hayo ya ubalozi na kuzungumza nao kujua hatima ya sakata hilo.
Baada ya makubaliano, familia hiyo ilielekea kwenye makazi hayo
ambapo wengine walifikia nje kwanza, Alex aliingia ndani kucheki
usalama, yaani kama mbwa hao walikuwa eneo hilo au la! Kabla wengine
hawajaingia.
“Kabla Alex hajamaliza kukagua, mbwa hao walimtoa mkuku. Ilikuwa na yeye ashambuliwe, ikabidi aruke ukuta ili kutoka nje.
“Kitendo hicho kilimtia uchungu bibi wa marehemu, yaani mama wa Alex
aliyekuwa kwenye gari ambapo alishindwa kuvumilia na kuangua kilio.
“Safari ya kuwaona wahusika wa ubalozi iliishia hapo. Wote walirudi nyumbani,” kilisema chanzo.
Chanzo chetu kiliendelea kudai kuwa baada ya kukaa kwa siku kadhaa, baba huyo wa marehemu alipigiwa simu na bosi wake akitakiwa kurudi kwani bado alitakiwa kuendelea kuishi mahali hapo akiwa msimamizi wa nyumba.

Habari zinadai kwamba, katika hali isiyokuwa ya kawaida, alipofika nyumbani hapo hakukuta mbwa hata mmoja.
Mpaka tunakwenda mitamboni balozi huyo hakupatikana lakini familia
nayo inasisitiza kwamba wanataka kukutana na viongozi wa ubalozi na
kujadili ni kitu gani kitaendelea.
0 comments:
Chapisha Maoni