Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas
ametupilia mbali pendekezo lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Marekani John Kerry la kutojiunga na mikataba ya kimataifa.
Mmoja wa maafisa wa Palestina leo ameripoti kuwa Mahmoud Abbas
amekataa pendekezo lililotolewa na John Kerry kwamba taifa la Palestina
liache kujiunga na makubaliano na mikataba ya kimataifa kwani
litazidisha hasira ya Israel. Afisa huyo amesema kwamba Abbas kupitia
njia ya simu amemsisitizia John Kerry kuwa, hatoacha kufuatilia suala
hilo kwani si takwa kubwa kwa Wapalestina na kwamba hawatotishwa na
vitisho vya Israel.
Maafisa wa Palestina wiki hii waliamua kutuma maombi katika Umoja wa
Mtaifa ili kujiunga na mikataba 13 ya kimataifa, ikiwa ni baada ya
Israel kukataa kuwaachilia huru mateka wa Kipalestina kama walivyokuwa
wamepatana.
0 comments:
Chapisha Maoni